Rais wa Argentina Cristina Fernandez de
Kirchner (kulia) akimsalimia mchezaji Lionel Messi mara baada ya kuwapokea leo
baada ya kurudi nchini kwao.
Mchezaji wa Argentina Lionel Messi leo
Julai 13, 2014 amepokelewa nchini kwao na Rais Cristina Fernandez de Kirchner
mara baada ya kushinda zawadi ya Mpira wa Dhahabu iliyotokana na kuwa mchezaji
bowa katika mashindano ya Kombe la Dunia yaliyomalizika jana nchini Brazili.
Mshabiki wengi wa soka wamempongeza sana mchezaji huyo kwa jinsi alivyocheza
japo timu yake haikuweza kuwashinda Wajerumani.
Rais
wa Argentina akimpa pongenzi meneja wa timu yao Alejandro Sabella.Pembeni ni
mchezaji Lionel Messi.
Viongozi wa nchi ya Argentina
wakifurahia jambo mapema leo mara baada ya kurudi nchini kwao.
Wachezaji
Messi akiwa ameshikilia medali yake ya dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora
katika mashindano ya kombe la dunia 2014 yaliyomalizika jana nchini Brazili na
kuifanya timu ya Ujerumani kuibuka washindi.