FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2014.....UJERUMANI VS ARGENTINA HUKO MARACANA BRAZIL



Mlinzi wa kati wa Ujerumani Mats Hummels alikosa kipindi cha pili katika mchezo dhidi ya Brazil kutokana na kusumbuliwa na mafua, lakini anatarajia kuwepo kwenye kikosi cha kwanza leo katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina kwenye dimba la Maracana, Brasilia huku Ujerumani kitarajia kukitumia kikosi chake kilichoiangamiza Brazil 7-1.

Naye mchezaji wa Argentina Angel Di Maria amerejea kwenye mazoezi baada ya kuumia paja lakini huenda akaanzia benchi.
Mshambuliaji Sergio Aguero amepona na yuko sawa baada ya kuuguza majeraha na huenda akacheza nafasi ya ama Ezequiel Lavezzi au Gonzalo Higuain huku wakitarajia kuwatumia wachezaji watatu mbele ambao ni Higuain, Aguero na Lionel Messi kama ambavyo walifanya mwanzoni mwa mashindano. 

Ujerumani v Argentia

Uso-kwa-uso 
  • Hii ni fainali ya tatu ya Kombe la Dunia kuzikutanisha Argentina na Ujerumani (ikiwepo ya Ujerumani Magharibi). Argentina walishinda fainali ya kwanza 3-2 mwaka 1986 lakini wakachapwa 1-0 kwenye fainali ya mwaka 1990.
  • Ushindi wa mwaka 1986 ulikuwa wa ushindi pekee kwa Argentina katika michezo sita ya Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani, na walitolewa katika fainali za 2006 na 2010.
  • Wanashikilia rekodi ya ushindi dhidi ya Ujerumani au Ujerumani Magharibi ni W1, D2, L3, ingawa moja kati ya sare hizo ilikuwa robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006 ambapo Ujerumani walishinda kwa matuta.
  • Kipigo cha Argentina cha 4-0 kutoka kwa Ujerumani kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ni kipigo chao kikubwa kuwahi kukipata katika mashindano hayo tangu mwaka 1974.
  • Walikutana hivi karibuni kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa mjini Frankfurt August 2012 ambapo Argentina walishinda 3-1.
Ujerumani 
  • Hii itakuwa ni fainali ya nane kwa Ujerumani au Ujerumani Magharibi kuchezakwenye Kombe la Dunia - ni rekodi mpya. Wameshinda fainali tatu na kupoteza fainali nne katika fainali zao saba za mwisho.
  • Ushindi wao kwa mara ya nne utawafanya kuwa sawa na Italia - ni Brazil pekee ambao wamelihifadhi Kombe la Dunia mara tano.
  • Ushindi utakuwa na maana kwamba watakuwa timu ya kwanza kutoka barani Ulaya kushinda Kombe la Dunia katika Amerika.
  • Wajerumani wamepoteza fainali nne zaidi ya timu yoyote. Hii inajumuisha fainali tatu walizopoteza kati ya nne za mwisho kucheza.
  • Ujerumani haijafungwa katika michezo yao 17 ya mwisho (W12, D5). Mchezo wao wa mwisho kupoteza ulikuwa kichapo cha 4-3 kutoka kwa Marekani kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki June 2013.
  • Katika michezo 12 ya Kombe la Dunia aliyocheza Thomas Muller amefunga magoli 10 na kutengeneza sita.
Argentina 
  • La Albiceleste imecheza michezo minne mila kufungwa katika fainali za mwaka huu - sawa na Uholanzi - na haikuwahi kufungwa katika hatua ya mtoano.
  • Lionel Messi ametengeneza nafasi 21 za magoli katika fainali za mwaka huu, ni nyingi kuliko mchezaji yeyote.
  • Messi amefunga katika michezo yake mitatu ya mwisho. Hajawahi kucheza michezo minne ya kimataifa bila goli tangu Alejandro Sabella alipochukua majukumu ya kuifundisha Argentina  August 2011.
  • Argentina waliondolewa na Ujerumani katika fainali za 2006 na 2010. Hakuna timu iliyoondolewa na timu moja katika hatua ya mtoano katika fainali tatu mfululizo.
  • Kikosi cha Argentina kina wastani wa umri wa chini ya miaka 29 - kama watashinda wataipiku Italia (2006) kama mabingwa wa Dunia mababu.
  • Ni timu pekee ambayo haijawahi kutoka nyuma kwenye fainali za Kombe la Dunia.