Lionel Messi amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano
LICHA
ya kupoteza mechi ya fainali na kukosa kombe la dunia mwaka 2014,
mshambuliaji wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi ameshinda tuzo ya
mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Messi
alionesha kiwango kikubwa katika hatua ya makundi akifunga mabao 4
katika michezo mitatu dhidi ya Bosnia, Iran na Nigeria, lakini nyota
yake ilififia baada ya kushindwa kufunga katika mechi za mtoano dhidi ya
Switzerland, Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani.
Katika
mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani, Messi alipoteza nafasi moja
muhimu, lakini muda mwingi alifanya jitihada za kutafuta upenyo bila
mafanikio.
Lionel Messi alipiga shuti, lakini alikosa bao katika mchezo wa fainali Maracana.
Baada
ya kipyenga cha mwisho, Messi alipokea tuzo yake ya mchezaji bora
akiwashinda nyota wa Colombia James Rodriguez, winga wa Uholanzi, Arjen
Robben na wachezaji watatu wa Ujerumani, Manuel Neuer, Bastian
Schweinsteiger na Thomas Muller.
Ndoto zimezima: Lionel Messi akiangalia chini baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Ujerumani.